Nuru FM

Azam Fc Yamsajili Sopu Mfungaji Bora Wa ASFC

4 July 2022, 3:49 pm

KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumsajili Mfungaji Bora wa Azam Sports Federation Cup (ASFC), Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miaka mitatu.

Sopu anakuwa mchezaji mpya wa nne na wa pili tu mzawa, baada ya kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji – pamoja wageni watatu, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.


Usajili wa safari hii ukifanywa na mmiliki wa timu mwenyewe, Yussuf Bakhresa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdukkarim Amin ‘Popat’.

Azam FC imeimarisha benchi la ufundi kwa kumrejesha aliyewaji kuwa mchezaji na kocha wake Msaidizi, Kali Ongala safari hii akipewa jukumu la kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, yaani feetness coach, huku ikiajiri kocha mpya wa makipa, Mspaniola, Dani Cadena ambaye amewahi kufundisha klabu za Sevilla na Real Betis za Hispania na nyingine za China na Asaudi Arabia akiwa na uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.