Nuru FM

NMB Yashiriki Futari Na Wateja, Wadau Wake Jijini Dar Es Salaam

18 April 2022, 9:10 am

Kwa kutambua thamani ya Wateja wao na umuhimu Mwezi wa Ramadhani, Benki ya NMB imeshiriki Futari na Wateja na Wadau mbalimbali wa Dar es Salaam na kuhudhuriwa Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakary Bin Zubery.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya Iftari Kwa wateja wa NMB wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mponzi amesema NMB imeamua kufanya tukio hilo kwasababu wanaamini kupitia mwenzi mtukufu, jamii kwa ujumla inastawishwa na Sala zinazotolewa wakati wa mwezi huu;

“Kwa msimu huu wa Ramadhani, Benki yetu ya NMB tunapenda kujumuhika na wapendwa wetu na wadau wengine mbalimbali wakati wa kufuturu kwani tunaamini kupitia mwezi huu tukufu, Jamii zetu zinastawishwa na sala za zati zinazotolewa wakati huu lakini pia baraka kwa watu wengi na Taifa kwa ujumla”

Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi amewasihi waislamu wote katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutafakari juu ya maadili yatakayowaunganisha Binadamu wote, upendo kwa familia, kufanya Toba na kuzidi kushiriki katika ibada.

 

Na hii siyo mara ya kwanza kujumuika na wateja wake katika ibada ya futari hivyo, wameamua kuendeleza utamaduni huo kwa kukutana na wadau wote wa NMB kujumuika wakati wa Iftari.

Mponzi amemshukuru Mufti Mkuu Sheikh Aboubakary Zubery, viongozi wote wa dini na serikali lakini pia wateja wote na wafanyakazi wa Benki ya NMB kwa kushiriki futari hiyo.

Kwa Upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakary Zubery amesema NMB wameonyesha upendo na kujali kwa kitendo cha kuandaa futari ambayo imewakutanisha watu mbalimbali na kujenga undugu;

“NMB mmethamini na kujali ndiyo maana mmeona umuhimu wa kuita watu mbalimbali kuja kufuturu futari ambayo inajenga undugu, inaweka watu karibu na watu kufurahi, hivyo viongozi wa NMB mmetuonyesha jinsi ambavyo mmekuwa na tabia nzuri na ya kuthamini”

Pia, Mufti Mkuu amesema wao kama Baraza kuu la Waislamu Tanzania wamekua wadau wakubwa kwa Benki ya NMB hivyo ametoa wito kwa Wananchi wote kufungua account za NMB kwani huduma zao ni bora zaidi .