Nuru FM

Makundi Maalum Yaaswa Kushiriki Zoezi La Sensa

18 April 2022, 9:06 am

Makundi maalum ya Wajane, Wagane, Yatima, Wazee na Watu wasiojiweza wametakiwa kujitokeza na kuhesabiwa siku ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi zitakazotumika katika kupanga mipango ya maendeleo.

 

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati wa zoezi la kugawa Iftar Kwa makundi hayo zoezi lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kitangiri ambapo Wazee, Yatima, Wajane, Wagane Kila mmoja alipata Tambi, Kilo 4 za Mchele, Kilo 3 za Sukari, Kilo 2 za Ngano.

Wajane waliongezewa Lita Moja ya mafuta ya kupikia, Misikitini ilipatiwa maboksi ya Tende,  Kisha kutembelea vituo vya watoto yatima na wasiojiweza vya Fenelisco kilichopo kata ya Ilemela, Hisani kata ya Buswelu na Nitetee cha kata ya Kiseke kugawa zawadi za Pasaka ambapo Juisi, Mafuta, Sukari, Mchele na Ngano vilitolewa  Kwa pamoja vikiwa na thamani ya jumla ya shilingi 38,500,000.

 

Kwa jumla ya idadi ya watu 882 ambapo akawataka kupokea sadaka hiyo Ili iwapunguzie adha Kwa siku zilizobaki za mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na Kwa waumini wa dini ya kikristo iwasaidie katika sherehe za kufufuka Kwa Yesu kristo maarufu siku ya Pasaka huku akiwasisitiza kuhakikisha wanajitokeza kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi kwani ni haki Yao na Kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali kupanga mikakati ya Utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

 

‘.. Ndugu zangu nawaomba mpokee hiki kidogo nilichojaaliwa na Mungu kiwasogeze katika mwezi huu mtukufu wa mfungo na Pasaka Kwa wenzetu wakristo, Lakini pia niwaombe kama Mheshimiwa Rais Samia anavyosisitiza mjitokeze kushiriki zoezi la Sensa ..’ Alisema

 

 

Aidha Mhe Dkt Mabula akawataka wananchi hao kuendelea kuwa wamoja na kuishi Kwa upendo kama Ilivyo Mila na desturi ya nchi sanjari na kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

 

Kwa upande wake Shekh wa wilaya ya Ilemela Shekh AbdulWarith Bin Juma amemshukuru mbunge huyo Kwa msaada alioutoa licha ya yeye kutokuwa muumini wa dini ya kiislamu lakini ameguswa kuwaunga mkono waislamu na mara zote amekuwa si mtu wa kujikweza na huwa anafikika kirahisi hivyo kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wake.

 

Moja ya wanufaika wa sadaka hiyo ambae pia ni  Yatima Rashid Balili mwanafunzi wa shule ya msingi Kayenze ndogo amempongeza Mbunge huyo sanjari na kumuomba kuendelea na moyo huo wa utoaji huku akimuombea Dua Kwa kidogo alichokipunguza katika kufanikisha zoezi hilo

 

Mbunge Mhe Dkt Angeline Mabula amekuwa akitoa sadaka ya futari na zawadi za Pasaka au Krisimasi Kila mwaka inapofikia ndani ya Jimbo lake na viunga vya jirani ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida aliojiwekea