Nuru FM

wazazi wajibikeni katika malezi

11 January 2021, 7:45 am

Wazazi na walezi mkoani iringa wametakiwa kushiriki vyema katika malezi na matunzo ya mtoto lengo likiwa ni kumstawisha mtoto katika hali ya maadili

Akizungumza na Nuru fm katibu tawala mkoa wa iringa Happiness seneda amesema kuwa anayo majukumu ya kimkoa lakini bado anashiriki vyema katika malezi na kusikiliza watoto wake pamoja na kuruhusu watoto kuuliza maswali .

katibu tawala mkoa wa iringa Happiness seneda

Nao baadhi ya wazazi wameeleza kuwa wazazi wanalo jukumu la kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano katika suala la malezi ya mtoto toka inapotungwa mimba mpaka anapozailiwa