Mpanda FM

Wazazi waaswa kuchangia miradi ya maendeleo shuleni

1 June 2023, 10:09 am

MPANDA

Wazazi wa watoto wanaosoma shule ya msingi Uhuru manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kujikita katika kuchangia miradi ya maendeleo ili kuwapunguzia wanafunzi changamoto zitokanazo na upungufu wa madawati pamoja na matundu ya vyoo.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa Kata ya Kashulili Magreti Shitunguru mara baada ya kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo na kuonekana baadhi ya michango iliyopitishwa na wazazi hao kukwama katika utekelezaji.

Kwa upande wa wazazi walioshiriki katika kikao hicho wamesema kuwa namna pekee ya kuiletea maendeleo shule hiyo ni ushirikiano wa pamoja katika ukamilishaji wa michango huku baadhi wakionyesha kuwa na mitazamo tofauti juu ya michango hiyo.

Shule ya msingi Uhuru ni miongoni wa shule za manispaa ya Mpanda na inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo pamoja na upungufu wa madawati.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayatamisemi

#WizaraYaElimu