Mpanda FM

Wafanyabiashara Shanwe kuneemeka na soko jipya

1 June 2023, 10:05 am

MPANDA

Wafanya biashara wa mtaa wa Shanwe kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wanatarajia kuanza kufanya biashara Juni mosi katika soko jipya, baada ya kupewa viwanja katika eneo la soko ililokuwa limetengwa kwa muda mrefu.

Wakizungumza na Mpanda Radio fm wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kupata eneo linaloweza kuwakutanisha wafanyabiashara wote. Awali walikuwa wakitumia vibanda majumbani kwa ajili ya kutoa huduma na wameushukuru uongozi wa kata kwa ajili ya kuwapatia ufumbuzi wa changamoto hiyo.

Akizungumza juu ya utaratibu uliotumika kugawa maeneo kwa wafanyabiashara, mwenyekiti wa mtaa Shanwe Mustapha Kimasa amesema jumla ya viwanja 316 vimetolewa kwa wafanyabiashara na wametenga eneo la kutupa taka, eneo la kujenga choo, na mfumo wa maji unaendelea kuletwa sokoni hapo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Shanwe Hafidhi Makolokolo amesema kutokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata wafanyabiashara kupanga eneo la barabarani wakati wa usiku, wameona ni vyema watenge eneo kwa huduma za muda wakati wanasubiri mchoro rasmi wa halmashauri.

#mpandaradiofm97.0

#manispaayampanda