Mpanda FM

Wakurugenzi watenge bajeti sekta ya michezo

30 May 2023, 10:10 am

MPANDA

Katibu tawala wa mkoa wa Katavi Hassan Rugwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha wanatenga bajeti ili kuwezesha sekta ya michezo.

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za msingi Tanzania [UMITASHUMTA ] amesema kukosekana kwa usimazi thabiti kunafanya kukosa msukumo na kuwataka kuweka kipaumbele kwenye sekta ya michezo.

Katika hatua nyingine Rugwa amewataka wakurugenzi kusimamia vyema vipindi vya michezo mashuleni na wakuu wa shule kuhakikisha maeneno ya shule yanapimwa ili kuepusha kubadilishiwa matumizi kwa viwanja vya michezo.

Awali aksoma taarifa ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2023/2024 afisa michezo wa mkoa wa Katavi Karoli Steven amesema jumla ya wanamichezo 385 wameshiriki michezo mbalimbali kutoka halmshauri mbalimbali ili kuwapata wataowakilisha mkoa wa Katavi katika mshindano ya kitaifa.

Michezo ya Umitashumta kitaifa inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Tabora Juni 04 mwaka huu na makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Isdory Mpango huku kaulimbiu ni michezo sanaa na taaluma kwa maendeleo ya uchumi na viwanda.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayasanaautamaduninamichezo

#wizarayatamisemi