Mpanda FM

Wananchi washauriwa kufanya usafi wa kinywa na meno

26 May 2023, 10:32 am

MPANDA

Jamii Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imeshauriwa kufanya vipimo vya meno, kufanya usafi wa kinywa kwa kuzingatia muda, kuepuka matumizi holela ya dawa zisizo za kitabibu ili kuepukana na magonjwa ya meno na kinywa kutoa harufu mbaya.

Ushauri huo umetolewa na daktari wa meno Kelvin Mremi kutoka hospitali ya manispaa ya Mpanda akizungumza na Mpanda Radio fm ambapo ameishauri jamii kuachana na matumizi holela ya dawa za meno, ili kuweka kinywa katika mazingira ya usafi.

Kwa upande wa wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema inahitajika njia sahihi ya kutibu meno huku wakisema magonjwa ya meno husababishwa na kutozingatia usafi wa kinywa .

Aidha Kelvin amesema kwa mujibu wa takwimu za wagonjwa wa meno waliohudumiwa kwa mwezi wa nne katika hospitali ya manispaa ni 145 huku wanawake wakiwa idadi kubwa na watoto wa jinsi ya kike walio chini ya umri wa miaka 18 ukilinganisha na wanaume.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayaafya