Mpanda FM

Wanne Wakamatwa na Meno ya Tembo Katavi

23 May 2023, 10:34 am

KATAVI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamewakamata watu wanne wakiwa na meno ya Tembo vipande 13 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 247.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame Amesema Katika tukio la kwanza watuhumiwa watatu Alex Ruben(45) Mkazi wa Kijiji cha Kapalamsenga Wilaya ya Tanganyika ,Masele Kasema(36) Mkazi wa Kijiji cha Sitalike Wilaya ya Mpanda na Nkamba Ntemula (45) Mkazi wa Maji Moto Wilaya ya Mlele walikamatwa wakiwa na vipande saba vya meno ya Tembo .

Kamanda Makame amesema watuhumiwa wamekamatwa na meno hayo ya tembo huko katika Mtaa wa Ikulu Kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda wakiwa wameyahifadhi ndani ya nyumba kwa ajiri ya kuyauza .

Amesema katika tukio la pili Askari wa Tanapa kwa kushirikiana wameweza kumkamata mhumiwa Michael Kisiba Mkazi wa Sumbawanga akiwa na vipande vya meno ya tembo vipande 11 ambavyo ni sawa na tembo sita .

Kwa upande Kamishina msaidizi Maneno Peter amesema kuwa idadi ya meno hayo ya tembo ni sawa na tembo saba wenye thamani ya Tshs 247.590 000 kwa fedha za Kitanzania .

#mpandaradiofm97.0

#jeshilapolisi

#maliasili