Mpanda FM

Sauti ya Katavi (Matukio)

19 May 2023, 8:16 pm

MPANDA

Watu wawili wamenusurika kifo mara baada ya kung’atwa na mbwa anayesadikika kuwa na kichaa katika Mtaa wa Maridadi Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Waliong’atwa na mbwa katika mtaa wa huo wa Maridadi ni Belta Baltazari mwenye umri wa miaka 6 ambaye amejeruhiwa kichwani na Said Mustapha ambaye ameng’atwa mguuni ambapo inasemekana mbwa huyo aliwakuta nyumbani majira ya jioni.

 BETORD BENJAMIN ANA TAARIFA ZAIDI

KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Katavi kushiriki kikamilifu katika masuala ya amani na ulinzi wa maeneo yao.

Akiwapongeza wakazi wa Eneo la Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kwa jitihada zao za Uzimaji Moto wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo iliyoungua, Mrindoko amesema kuwa ni vizuri kwa Wananchi kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa Amani pindi vinapotokea katika maeneo yao.

Mwandishi wa Mpanda radio  FM Henry Mwakifuna alikuwepo wakati Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akitoa Wito huo na hii hapa ni Taarifa yake.

TANGANYIKA-KABUNGU

Wakazi wa vijiji vya kata ya kabungu halmshauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wametakiwa kutunza vyanzo vya mji ikiwa ni Pamoja na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika milima.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha kabungu kata ya kabungu Meneja wa wakala wa misitu wilaya ya Tanganyika TFS SAIMON PETER amewataka wananchi hao kutunza misitu Pamoja na vyanzo vya maji kwa faida ya vizazi vya baadae MWANAHABARI WETU BEN GADAU KUTOKEA HUKO ANATUJUZA UNDANI WA TAARIFA HII.

KATAVI

Waandishi wa Habari Mkoani Katavi wameombwa kuandika habari kuhusu Ugonjwa wa malaria ili kupunguza maambukizi katika jamii.

Hayo yamebainishwa na kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Katavi Mohamed Kassimu Mpunji katika semina ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari za ugonjwa wa Malaria ambapo amesema kuwa Mkoa wa Katavi unasilimia 8.1 katika maambukizi wa ungonjwa huo.

Kwa undani wa Habari hii tuungane na john benjamin

MPANDA

Wananchi wa kata ya Kawajense manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamenufaika na ajira kupitia mradi wa boost unaoendelea kwenye kata hiyo.

Kupitia mradi huo baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamejitokeza kuchangamkia fursa za upishi na ufundi huku idadi kubwa ya Saidia fundi ikihitajika.

GLADNESS RICHARD Anakuja na undani wa taarifa hiyo.

SONGWE.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema ipo katika mkakati wa kuboresha makumbusho ya kimondo cha Mbozi yaliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Lengo likiwa ni kuongeza mambo ya kale baada ya kuendelea kukusanya na kupata taarifa kutoka kwenye jamii ya eneo hilo juu ya uwepo wa vitu vingi vya kale nje ya eneo hilo ambavyo vina historia inayoweza kuwa sehemu ya vivutio vya utalii katika makumbusho hayo.  MWANDISHI WETU  WILLIAM LIWALI. Anatupa undani wa taarifa hiyo kutoka chumba cha Habari

DODOMA

Serikali imetakiwa kuwa mstari wa mbele kuvilipa vyombo  vya Habari katika matangazo mbalimbali yanayotolewa  na serikali  pindi hivyo vinapofanya kazi ili kuviwezesha kutekeleza majukumu yake

Kauli hiyo imetolewa leo na Mbunge wa viti maalm Ester Bulaya wakati akichangia bajeti ya teknologia ya Habari na Mawasiliano katika mwaka wafedha 2022/2023 VERONICA MABWILE AMEFATILIA BUNGE HILO KUTOKA CHUMBA CHA HABARI ANATUKUFIKISHIA TAARIFA HITO

IRINGA

Mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la Jason Akwilo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita amefariki dunia baada ya kuzama kwenye kisima kilichopo eneo la vinyunguni mtaa wa Lumwago Mjini Mafinga.

Kwa mujibu wa ripoti ya jeshi la polisi Nchini Kuanzia Januari hadi Aprili 2023 kumejitokeza matukio ya watoto 37 kufa maji kwa kusombwa na maji na kutumbukia kwenye visima au mashimo yaliyojaa maji Katika mikoa mbalimbali HUYU HAPA ANNA MILLANZI ANATUARIFU JUU YA TAATIFA HII KUTOKEA MKOANI IRINGA.

NA    KATIKA MICHEZO

Kikosi cha yanga kimeingia nchini mapema leo hii kikitokea Afrika ya kusini kwenye mashindano ya kombe la shirikisho barani afrika, na kimataifa Al Ahly kuminyana na Esperance leo kwenye nusu fainali ya pili kombe la klabu bingwa barani Afrika.

Huyu hapa mwanamichezo wetu Killian Samwel na taarifa Zaidi za michezo.