Mpanda FM

CCM Katavi yakemea ukatili kwa watoto

19 May 2023, 8:09 pm

KATAVI

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi [CCM] mkoa Katavi imeeleza kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vinavyoendelea kujitokeza vinachangiwa na utumikishaji wa watoto katika shughuli za ujasiriamali pamoja na utelekezaji wa familia .

Hayo yamebainishwa na katibu wa jumuiya ya wanawake mkoa wa Katavi Jenifer Chinguile kwa niaba ya katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa Bashiru Kambarage wakati akizungumza na kituo hiki ofisini kwake na kusema ukatili unaozungumziwa kwa sasa unaanzia kwenye familia kutokana na wazazi au walezi kushindwa kutimiza majukumu ikiwemo kuwahudumia watoto

Kwaupande wa wazazi mkoani Hapa wamesema kuwa ili vitendo viweze kudhibitiwa katika jamii ni muhimu kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji taarifa kwa jeshi la polisi ili kusaidia washukiwa wamatukio ya ukatili kuchukuliwa hatua

Miongoni mwa madhara ya vitendo vya ukatili kwa watoto ni Pamoja mimba za utotoni ,mtoto kuathirika kisaikolojia ,vifo,

Pamoja na migogoro katika jamii

#mpandaradiofm97.0

#ccm