Mpanda FM

Zaidi ya mbwa 621 wauwawa Katavi

17 May 2023, 7:08 pm

MPANDA

Zaidi ya mbwa 621 wameuawa kufuatia zoezi lililofanyika kwa awamu nne la kuangamiza mbwa wasio na makazi maalum ili kuondoa mrundikano wa mbwa wenye vichaa ndani ya manispaa ya Mpanda.

Hayo yamesemwa na Afisa Mifugo wa manispaa ya Mpanda Tulinalo Nswila ambaye amesema kuwa zoezi hilo limefanyika katika kata zote za manispaa ya Mpanda na kufanikiwa kuwauwa mbwa hao.

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa zoezi hilo ni zuri na liwe endelevu kwenye mitaa yao huku wakiiomba serikali kutoa chanjo kwa wafugaji wa mbwa.

Wafugaji wa mbwa wametakiwa kufungia mifugo yao na kuhakikisha kila mwaka wanapata chanjo .

#mpandaradiofm97.0

#wizarayamifugonauvuvi