Mpanda FM

Wananchi waomba elimu sahihi ya matumizi ya gesi

17 May 2023, 7:07 pm

KATAVI

Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wameomba kupatiwa elimu juu ya matumizi sahihi ya nishati mbadala ya (gas).

Wakizungumza na Mpanda Radio FM wamesema watu wengi wamekuwa wakitumia nishati hiyo kwa mazoea bila kuwa na elimu sahihi ya matumizi yake .

Kwa upande wake afisa habari msaidizi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Katavi Catherin Sembagi amesema wananchi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kukagua mara kwa mara vifaa wanavyotumia kwenye nishati mbadala ili kuepusha kuvuja kwa gesi na kutokea kwa moto.

Matumizi ya nishati mbadala nchini yamekuwa yakilenga kampeni mbalimbali za utunzaji wa mazingira.

#mpandaradiofm97.0

#jeshilazimamotonauokoaji

#wizarayanishati