Mpanda FM

Sauti ya Katavi (Matukio)

17 May 2023, 7:16 pm

KATAVI-TANGANYIKA

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kasinde wameutaka uongozi wa kijiji hicho kutolea ufafanuzi  utaratibu uliopo katika uchimbaji wa madini ya COPPER yaliyopo katika mlima wa  kijijini hapo.

Hii inajiri mara baada ya uwepo wa taarifa za uwepo wa fununu za mwekezaji katika kijiji hicho kitendo ambacho wananchi wanakiri hawajapewa taarifa kutoka katika uongozi wa kijiji hicho.

Mwanahabari wetu BEN GADAU amepiga kambi katika kijiji hicho na hapa anazungumza na wananchi hao.

MPANDA

Wafanyabiashara wa Samaki wabichi wameshauriwa kuzingatia ubora na ukubwa wake ili kuepuka adhabu zitolewazo na serikali kwa kuuza samaki chini ya kiwango kinachotakiwa na serikali.

Samaki wanaotakiwa kisheria ni kuanzia inch tatu na kuendelea na Samaki alie chini ya inch tatu ni mchanga hivyo bado muda wa kuvuliwa Mwandishi wetu GLADNESS RICHARD Anatuarifu undani zaidi.

MPANDA

Baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF wanaofanya kazi ya kutengeneza Barabara za mitaa katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wameishukuru serikali kuwawezesha kuwapa ajira za muda

Wakizungumnza na sauti ya Katavi wakiwa katika shughuli yao ya ujenzi wa barabara ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda wamesema kuwa kupitia ajira wanazozipata zimekuwa zikiwasaidia kuwainua kiuchumi kwa kujipatia kipato, John benjamin anakuja na undani wa Habari hii.

KATAVI

Jumuiya ya wazazi mkoani Katavi kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM imeeleza kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vinavyoendelea kujitokeza kwa sasa vinachangiwa na utumikishaji wa watoto katika shughuli za ujasiriamali pamoja na utelekezaji wa familia .

Hayo yamebainishwa na katibu wa Jumuiya ya wanawake mkoa wa Katavi Jenifer Chinguile  kwa niaba ya katibu wa jumuiya ya wazazi  kupitia chama hicho Bashiru Kambarage wakati akizungumza na kituo hiki ofisini kwake  na kusema kuwa ukatili unaozungumziwa kwa sasa unaanzia kwenye familia kutokana na wazazi au walezi kushindwa kutimiza majukumu yao.

 VERONICA MABWILE anatuletea taarifa kamili.

DODOMA.

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amesema elimu iliyotutoa tulipotoka kama taifa na kutufikisha mahali tulipo haiwezi kutupeleka kule tunakotaka kwenda hivyo lazima kuwe na mabadiliko makubwa kwenye mitaala ya elimu.

Shigongo amesema hayo bungeni na kueleza kwamba amefurahishwa kuona katika mswada wa mtaala mpya wa elimu kuna masomo ya coding kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya chini. Huyu hapa ANNASTAZIA FILIMBI kutoka chumba cha habari ametuandalia taarifa hiyo.

DAR ES SALAAM

Lazaro Nyachuma [66] mkazi wa Tabata jijini Dar es salam ameuwawa kwa kuchomwa kisu na mjukuu wake Nasibu Limba maarufu kama Romanus [18] huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugomvi wa  mara kwa mara ndani ya familia.

Mke wa marehemu ameeleza kuwa ugomvi uliosababisha kifo cha mume wake na mjukuu ulianza baada ya babu kutoridhishwa na majibu aliyopewa na mjukuu wake

 Betord benjamin kutoka chumba cha habari anatuletea kisa hicho chenye majonzi ndani yake.

DAR ES SALAAM.

Waziri mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameunda tume itakayosikiliza hoja zote zilizoibuliwa kwenye mkutano wake alioufanya na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo kufuatia mgomo ulioanzishwa na wafanyabiashara hao.

Tume hiyo imelazimika kuundwa ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabishara wa soko hilo hadi kulazimika kufanya  mgomo kwa kufunga maduka .

Taarifa iliyoandaliwa na dawati la Habari inasomwa studioni na WILLIAM LIWALI.

MICHEZO

Ngumi Jiwe kuanza safari kesho ya kuelekea Dubai kwa ajili ya pambano lake ambalo litapigwa Mei 20, JKT QUEENS yatawazwa kuwa bingwa ligi ya wanawake msimu wa 2022/23 na Kimataifa Manchester City kuminyana na Real Madrid.

Killian Samwel anakuja na kina cha taarifa zote za michezo.