Mpanda FM

Wananchi wanawajibu wa Kushiriki Kuepusha Ajali

12 May 2023, 5:46 am

KATAVI

Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wametoa maoni juu ya ushiriki wao katika kuepusha ajali pindi wanavyokuwa katika vyombo vya usafiri

Wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wanawajibu wa kupaza sauti kwa dereva ambaye hazingatii sheria ya usalama barabarani ikiwemo mwendokasi na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi .

Reopord Fungu ni Mratibu mwandamizi jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Katavi amesema kuwa wanananchi wanawajibu wa kushiriki kuzuia ajali na amewaomba kutoa ushirikiano kwa kupaza sauti na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani .

#mpandaradiofm97.0

#UsalamaBarabarani