Mpanda FM

Mwanga Awataka Wazazi Kuendelea Kuchangia Chakula Shuleni

9 May 2023, 8:13 pm

MLELE

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amewataka wazazi na walezi Wilayani humo waendelee kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi wote kwa shabaha ya kuinua kiwango cha ufaulu.

Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Inyonga katika Mkutano wa hadhara ulilofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Inyonga iliyopo Halmashauri ya Wilaya Mlele.

Aidha amewaelekeza viongozi wa Serikali za Vijiji kuendelea kutekeleza mkakati wa utoaji wa chakula shuleni kwa kuwamasisha wazazi kuchangia kwa mujibu wa sera ya Elimu bila malipo.

Mapema akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji Alfred Sungura, ameelezan kuwa Halmashauri ya Wilaya Mlele inayosimaia utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya Shule Zahanati na Vituo vya Afya kwenye Halmashauri.

Sungura amebainisha kuwa yapo maendeleo makubwa kwa kipindi cha miaka mitano, hiyo kwa upande wa Shule za Msingi kulikuwa na Shule 13 mwaka 2019 lakini sasa zipo shule za Msingi 25,upande wa Shule za Sekondari zilikuwepo tatu kwa sasa zipo Shule kumi.

#mpandaradiofm97.0

#mleledistric

#wizarayaelimu