Mpanda FM

Katavi Yataraji Kuzalisha Milioni 15.5 za Tumbaku

5 May 2023, 5:04 am

NSIMBO

Mkoa wa Katavi unatarajia kuongeza uzalishaji wa zao la Tumbaku kwa msimu huu kwa kuzalisha jumla ya kilo Milioni 15. 5.

Akizungumza wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya kilimo cha Tumbaku Mkoa wa Katavi Meneja Mkoa wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Genwin Swai amesema msimu wa kilimo 2021/2022 makisio ya awali ya uzalishaji yalikuwa ni kilogramu 8,220,000 hata hivyo hadi kufikia msimu wa kilimo ulipo malizika ziliweza kununuliwa kilogramu 6,663,136 zenye thamani ya shilingi Bilioni 26 madeni ya pembejeo yalikuwa Bilioni 13. 9.

Katika hatua nyingine Amezitaja changamoto zilizopo ni wakulima kuendelea kuchanganya tumbaku ambapo tumbaku yenye uzito wa juu huchanganywa na tumbaku yenye ubora wa chini ili kudanganya wanunuzi au kuchanganya vitu visivyo tumbaku (Ngulai)

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahimiza watumie wakutumia fursa zilizoletwa na Serikali za kuwaletea wakulima ushindani wa wanunuzi hivyo wazitumia vizuri furusa hiyo kwa kuwa waaminifu na waachane na tabia ya kuchanganya tumbaku yao na vitu ambavyo sio tumbaku .

Aidha mrindoko amewaonya wakulima kuacha tabia ya kutorosha tumbaku kwani na watakao bainika na kukamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo ya kutaifishwa tumbaku waliyokuwa wanataka kuitorosha .

#mpandaradiofm97.0

#wizarayakilimo

#tobaco