Mpanda FM

Wananchi Waomba Elimu ya Lishe kwa Wajawazito

2 May 2023, 9:18 pm

KATAVI.

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameomba kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito.

Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamesema hawapatiwi elimu juu ya lishe bora kwa mama mjamzito zaidi ya kuishia kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi[VVU] huku wakisema vyakula vingine mama mwenyewe anachagua .

Kwa upande wake Afisa lishe wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Mwanaidi Salim amesema mama mjamzito anatakiwa apate vyakula katika makundi yote matano kwani inamuongezea uzito mama na kuzuia mtoto kudumaa huku akisema kwa siku mama mjamzito anatakiwa apate milo minne [4].

Mwanaidi amewataka wajawazito kujitambua na kuzingatia kula kwani wamepewa jukumu la kubeba viumbe hai huku akiwaasa pindi wanapo jihisi wajawazito waende kituo cha afya kwaajili ya kupatiwa elimu ya lishe bora na elimu juu ya dalili za hatari.