Mpanda FM

Katavi yapanda miti milioni 6 tangu mwezi Februari

2 May 2023, 9:41 am

NSIMBO

Serikali mkoa wa Katavi imesema miti milioni sita imepandwa toka mwezi wa Februari mwaka huu katika halmashauri za mkoa wa Katavi.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amebainisha hayo wakati akizungumnza na wananchi wa Kijiji Cha Isinde halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya shughuli za upandaji miti katika shule ya msingi Isinde.

Amesema kuwa tangu Shughuli Mbalimbali za upandaji wa miti zianze katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi hadi sasa kuna miti zaidi ya Milioni 6 imepandwa katika mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Maagizo ya viongozi wa juu ya suala la utunzaji wa Mazingira

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani amsema kuwa halmashauri hiyo imekuwa ikitekeleza agizo la Upandaji miti kwa kupanda miti katika sehemu mbalmbali za halmashauri ya Nsimbo

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe ambae pia ni Makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mazingira na Maji amesema kuwa kamati hiyo imekuwa ikisistiza suala la uhifafadhi wa mazingira ikiwa nipamoja na Upandaji wa Miti.