Mpanda FM

Vijana na Watu wenye Ulemavu Wasumbufu Kulipa Mikopo Asilimia 10

30 March 2023, 3:36 pm

MPANDA

Vijana na watu wenye ulemavu wametajwa kuwa ni miongoni mwa makundi sumbufu kwa kutolipa mikopo ya 10% ambayo inatolewa na halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa manispaa ya Mpanda Marietha Mlozi Na kuainisha kuwa kuna vikundi vilivyopewa mikopo tangu mwaka 2017,2018 na 2019 mpaka sasa hawajamaliza marejesho.

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa changamoto wanayokutana nayo ni kutokuwa na mitaji ya kudumu na kujirekebisha ili kuweza kulipa mikopo.

Aidha Marietha amewashauri vijana kujishughulisha na biashara zenye tija ili waweze kulipa mikopo kwa wakati.