Mpanda FM

CHAKUHAWATA Mpanda Waaswa Kuelimisha Maadili kwa Walimu

29 March 2023, 8:26 am

MPANDA

Viongozi wa chama cha kulinda na kutetea haki za walimu Tanzania (CHAKUHAWATA) wilaya ya Mpanda wametakiwa kuelimisha maadili na miiko ya kazi kwa walimu.

Kauli hiyo imetolewa na katibu msaidizi wa tume ya utumishi ya walimu wilaya ya mpanda Benson Ngamilo wakati wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wa chama wilaya ya mpanda ambapo amesema viongozi wanapaswa kuwalea wanachama ili kuona manufaa ya uwepo wa chama.

Kwa upande wao wagombea walioshindwa kupata kura za kwenye uchaguzi huo wamekiri kuridhika na matokeo huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi waliopatikana katika mchakato huo.

Aidha viongozi wapya waliopata ridhaa ya kuwa viongozi katika chama hicho wameshukuru kwa kupata nafasi huku wakiahidi kuwatumikia wanachama waliowachagua

Uchaguzi huo umehudhuriwa na viongozi wa matawi 52 katika wilaya ya Mpanda ambapo mwenyekiti wa chama hicho kwa sasa ni Datus Mwakasanga ambaye amepata kura 26 dhidi ya Benjamin Masai aliyepata kura 25.