Mpanda FM

“Wanafunzi wafundishwe lugha kwanza”Msonde.

25 March 2023, 12:25 am

KATAVI
Walimu wa shule za sekondari na msingi mkoani Katavi wametakiwa kujikita kuwafundisha lugha wanafunzi Ili kutengeneza mazingira rafiki ya uelewa katika masomo.

Hayo yamesemwa na Naibu katibu mkuu ofisi ya rais Tamisemi Dk. Charles Msonde katika kikao kazi na taasisi za elimu mkoani hapa amesema walimu wengi wamekuwa wakifundisha Kwa mazoea jambo ambalo linarudisha nyuma taaluma Kwa wanafunzi huku akisema njia Bora ya ufundishaji ni mwanafunzi kujua lugha kwanza.

Aidha baadhi ya wakuu wa shule waliohudhuria kikao hicho wamekiri kupokea maelekezo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi Lengo likiwa ni kuinua taaluma Kwa wanafunzi mkoani hapa.

Afisa elimu mkoa wa Katavi Upendo Rweyemamu amesisitiza walimu na viongozi kuwa na umoja ili kufikia mafanikio ya elimu katika ngazi ya mkoa.

Kikao hicho kimehudhuliwa na taasisi za elimu ngazi ya msingi na sekondari mkoani hapa.