Mpanda FM

Wanawake wawe Mstari wa mbele, Mtoto wa Kike Kupata Elimu

20 March 2023, 4:56 pm

KATAVI

Wanawake Mkoani Katavi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha watoto wa kike juu ya umuhimu wa elimu sambamba na kuwaeleza fursa zinazotolewa na serikali ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao .

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati wa kongamano la wanawake kuelekea siku ya mwanamke iliyofanyika machi 8 mwaka huu na kusema kuwa mkoa wa katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo watoto wakike wanashindwa kupata haki ya elimu kutokana sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni.

Kwaupande wake Mbunge wa Viti maalum Tusker Mbogo akizungumza wakati wa kongamano hilo amesema kuwa ni vyema mwanamke akatumia nguvu yake ya ushawishi kwa kuwapa elimu wasichana juu ya namna ya kupambania ndoto zao ikiwemo elimu