Mpanda FM

Wananchi Waendelea Kuaswa Kuchukua Tahadhari Dhidi ya Ugonjwa wa Surua

9 March 2023, 12:23 pm

KATAVI.

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari juu ya mripuko wa ugonjwa wa surua na kutakiwa kufika kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya pindi wazionapo dalili za ugonjwa huo.

Wito huo umetolewa na mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa Katavi Stephano Kahindi wakati akifanya mahojiano na mpanda redio fm na kusema kuwa bado visa vya ugonjwa wa surua vinaendelea kuripotiwa mkoani hapa huku akiwataka wananchi kufika mapema kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mara tu baada ya kuona dalili za ugonjwa.

Nae afisa ufuatiliaji na tathmini wa mradi wa USAID afya yangu mkoa wa Katavi Agrey Mbilinyi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa idara ya afya wakati zoezi la chanjo likiendelea kufanyika.

Hadi sasa ni takribani visa 132 vilivyoripotiwa vya ugonjwa wa surua katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika, na vifo 13 vilivyoripotiwa halmashauri ya mpimbwe vilivyotokana na ugonjwa wa surua.