Mpanda FM

Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Wanawake Waaswa Kupinga Vitendo vya Ukatili

9 March 2023, 1:08 pm

KATAVI

Katika kuelekea  siku ya mwanamke Duniani march 8 mwaka huu ,Wanawake  Mkoani Katavi wametakiwa kupinga vitendo vya uvunjifu wa maadili sambamba na vitendo ukatili kwa wanawake na watoto ili kuendelea kutengeneza jamii yenye maadili na usawa

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko  wakati  wa kongamano la wanawake lililofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda na kusema kuwa mwanamke anayo nafasi kubwa ya kuhakikisha vitendo vya ndoa za jinsia moja na ubakaji vinaisha katika jamii kwa kuendeleza malezi yanayotokana na  dini

Kwa upande wao washiriki wa kongamano hilo wamesema kuwa vitendo hivyo vianapaswa kuendelea kupingwa kwa nguvu moja ili kuendelea kuitengeneza jamii yenye madili

Kilele cha siku ya wanawake duniani  kinatarajia kufanyika marchi 8 mwaka huu katika wilaya ya Tanganyika ,viwanja vya shule ya msingi Majalila ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa