Mpanda FM

Wananchi Waaswa Kuchukua Tahadhari ya Surua

22 February 2023, 6:33 pm

KATAVI

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa surua ulioibuka katika halmashauri ya mpimbwe mkoani katavi.

Hayo yamesemwa na Dr solomon solomoni wakati akizungumza na Mpanda redio fm na kuainisha kuwa mlipuko wa surua unaathiri zaidi watoto chini ya umri wa miaka mitano huku akisema kuwa unatokana na virusi vya rubella.

Aidha solomoni ametaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo wa surua kuwa ni mafua,kutokwa na vipele katika ngozi huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Dr solomoni solomoni kutoka ofisi ya mganga mkuu mkoa wa Katavi amethibitisha kuibuka kwa virusi vya surua katika halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.