Mpanda FM

Wananchi Kapanga Wamlilia Mrindoko

16 February 2023, 4:51 am

TANGANYIKA

Wananchi wa kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese wilayani Tanganyika wamemuomba mkuu wa mkoa wa katavi kuwasaidia changamoto zinazowakabili katika kijiji hicho.

Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa alipokuwa anakagua miradi iliyojengwa kupitia Fedha za Hewa ya ukaa kijijini hapo wameomba kusaidiwa mnara kwaajili ya mawasiliano na kuwawezesha vijana kupata elimu ya ujasiliamali.

Aidha Mkuu wa mkoa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amemuagiza mkuuwa wilaya ya Tanganyika kuorodhesha maeneo yote yenye changamoto ya mtandao wilayani hapo ili taarifa iwasilishwe wizara husika.

Pia Mwanamvua ametoa shilingi million moja kwaajili ya kuwezesha vikundi viwili vya wajasiliamali huku akimuagiza mkurugenzi wa wilaya hiyo, kupeleka wataalamu kutoa elimu ya ujasiliamali kijijini hapo.