Mpanda FM

Umaskini Wachangia Elimu Kuwa Chini Katavi

16 February 2023, 6:10 am

KATAVI
Umaskini, uelewa mdogo wa Wazazi na Walezi ni miongoni mwa sababu zinazoelezwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda kupelekea Elimu kuwa Chini katika mkoa wa Katavi.

Wakizungumza na Mpanda Radio wakati wakitoa maoni kuhusu ubora wa elimu Wananchi wamesema Wapo wanaowatumia watoto katika utafutaji wa Riziki na kushindwa kuendelea na masomo ikiwemo kuelekea machimboni.

Mratibu wa mradi wa shule Bora Mkoa Kwa katavi Bakari Geni amesema Mradi wa shule Bora umekuja kutoa suluhisho la elimu bora kwa Watoto wote kwa kuwezesha kila mtoto kupata msingi mzuri katika elimu yake ya awali na msingi.

Mradi wa Shule bora ni mpango wa Elimu wa Serikali ya Tanzania kwa Ufadhili wa Mfuko wa UKAID wa Uingereza unaolenga kuunga mkono uboreshaji wa Elimu ya msingi Tanzania