Mpanda FM

Wafanyabiashara Wapongeza Ukaguzi wa Mizani

10 February 2023, 12:29 pm

KATAVI

Wafanyabiashara Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamepongeza zoezi la ukaguzi wa mizani Wanazotumia katika biashara.

Wakizungumza na Mpanda radio Fm wafanyabiashara hao Wakati wa zoezi la ukaguzi katika ofisi za kata ya Makanyagio likiendelea wamesema zoezi la ukaguzi wa mizani linafaida kwenye biashara ikiwemo kuwa na usawa wa vipimo kati ya mfanyabiashara na mteja Na kutaka zoezi kuwa endelevu ili kurahisha ufanyaji wa biashara.

Kwa upande wake Mkaguzi wa vipimo kutoka ofisi ya wakala wa vipimo mkoa wa Katavi Rajabu Komba ameeleza umuhimu wa zoezi hilo huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza kukagua mizani zao pindi wanapopata taarifa za ukaguzi.

Zoezi hilo la ukaguzi wa mizani bado linaendelea mkoani hapa Ambapo Mkaguzi wa vipimo kutoka ofisi ya wakala wa vipimo mkoa wa Katavi anatembelea kata zilizopo Manispaa ya Mpanda kwa ajili ya ukaguzi.