Mpanda FM

Umuhimu wa Mjamzito Kujifungua Hospitalini

10 February 2023, 12:38 pm

KATAVI

Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wameeleza umuhimu wa mama mjamzito kujifunguwa kwenye kituo cha afya.

Wakizungumza na Mpanda radio Fm Wananchi hao wamesema mama mjamzito kujifungua nyumbani kunaweza kuleta hatari ya kupoteza uhai wa mama na mtoto.

Kwa upande wake Mratibu huduma ya afya uzazi na mtoto mkoa wa Katavi Elida Machungwa amesema kuna baadhi ya wajawazito ambao bado wanajifungua kwa wakunga na waganga wa jadi jambo ambalo linaweza kuhatarisha uhai wa mama na mtoto huku elimu ikiwa inahitajika kuendelea kutolewa.

Kwa mjibu wa Elida Machungwa katika kipindi cha mwaka 2022 zaidi ya akina mama 700 mkoani Katavi wamejifunguwa nyumbani.