Mpanda FM

Zaidi ya Heka 200 za Mazao Zaharibiwa na Mvua Nsimbo

8 February 2023, 12:26 pm

NSIMBO

Zaidi ya heka 200 za mazao ya chakula na biashara zimeharibiwa na mvua iliyonyesha January 31 mwaka huu katika Kijiji cha Ikolongo kata ya mtapenda Halmashauri ya Nsimbo Mkoani katavi.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Mtendaji wakijiji cha Ikolongo Dickisoni Benedicto amebainisha uharibifu uliojitokeza kutokana na mvua hiyo kunyesha na kueleza kuwa jumla ya heka 225 za mazao zimeharibiwa .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wameeleza juu ya athari zilizojitokeza kutokana na mvua hiyo katika mashamba yao.

Diwani wa kata hiyo Elieza Fyula ameiomba serikali Kuchukua hatua za dharura ili kuwasaidia wananchi hao.