Mpanda FM

Wazazi Ambao Hawajawapeleka Watoto Shule Wachukuliwe Hatua

8 February 2023, 12:11 pm

ATAVI

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka viongozi kuwachukulia hatua za kisheria wazazi ambao watoto wao wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza lakini bado hawajaripoti shuleni hadi hivi sasa

Ameyasema hayo Februarymosi 2023, katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria na kueleza kuwa zaidi ya wanafunzi 2000 hawajaripoti katika shule ambazo wamepangiwa.

Kwa upande wa wananchi wamesema kuwa ni sahihi wazazi hao wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu ya uzembe kwa kutowapeleka watoto hao shule.