Mpanda FM

Uzinduzi wa REAT Mkoani Katavi

8 February 2023, 12:19 pm

KATAVI

Wafanya kazi wastaafu mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kuwa wazalendo na kuipenda nchi na kutoa mawazo chanya kwa jamii inayowazunguka.

Hayo yamesemwa na afisa maendeleo Anna Kumbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko Katika uzinduzi wa chama cha wastaafu kilicho zinduliwa mkoani hapa cha retayard Asosiation of Tanzania [ REAT] ambacho kinawaunganisha wastaafu hao ili kutetea na kulinda maslahi yao.

Mwenyekiti wa chama hicho Zabadi Mwakasungura amesema kazi ya chama hicho ni kutetea maslahi ya wafanya kazi wastaafu, ambapo chama hicho kitaweza kusadia kudai haki za mstaafu ambapo hadi sasa jumla ya wanachama 11 tayari wameshajiunga na kuwaomba wafanyakazi wengine kujiunga na chama hicho .

Kwa upande wao wanachama wa chama hicho wamesema kuwa wanashukuru kuwepo kwa chama hicho kwa kuwa kinawaunganisha na kusaidia kutatua changamoto zinazowakumba kama madai ya pesheni na kiinua mgongo .