Mpanda FM

Jumla ya Watu 222 Waugua Surua Mlele

8 February 2023, 12:15 pm

KATAVI
Jumla ya visa 222 vya wagonjwa wa surua vimeripotiwa ndani ya siku 55 wilayani Mlele mkoani Katavi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati wa kikao cha kujadili tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe, mkakati wa kuzuia magonjwa ya mlipuko, na utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto mkoa wa Katavi amesema jumla ya kata 11 wilayani humo ndizo zilizoathiriwa na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mratibu wa ufuatiliaji wa Magonjwa mkoa wa Katavi Dr. Karume Ramadhani amesema kufuatia visa hivyo wamejipanga kutoa elimu kwa jamii namna ya kujikinga na ugonjwa huo sambamba na wanafunzi ambao wameonesha dalili ya ugonjwa huo kusimamishwa masomo ili kupata matibabu.

Ugonjwa wa Surua unakinga ambapo chanjo yake utolewa kwa mtoto akiwa na umri wa miezi 9 na kurudiwa akiwa na miezi 18.