Mpanda FM

Kesi Zimalizwe kwa Usuluhishi Kuokoa Muda

7 February 2023, 10:19 pm

KATAVI

Wananchi mkoani katavi wameshauriwa kumaliza kesi za madai kwa njia ya usuluhishi ili kuondoa gharama na kutopoteza muda.

Hayo yamesemwa na Hakimu mkazi mkuu mfawidhi mkoa katavi Gway Sumaye alipokuwa akitoa hotuba katika hitimisho la wiki ya sheria ambapo amesema miongoni mwa kesi zinazochukua muda mrefu mahakamani ni kesi za madai.

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa wamejifunza kufanya usuluhishi kuanzia ngazi ya chini kabla ya kwenda mahakamani.

Maadhimisho ya wiki ya sheria yalianza tarehe 23 Januar 2023 na kuhitimishwa februar 1, 2023 huku kauli mbiu ikiwa ni ‘‘umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau’’