Mpanda FM

Wauza Vyakula Waaswa Kuzingatia Usafi.

17 January 2023, 5:39 pm

KATAVI
Wananchi manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewaomba Wauzaji wa vyakula migahawani kuzingatia kanuni za usafi ili kuepukana na Magonjwa ya milipuko yanayoweza kuwapata Wateja.

Wakizungumza na Mpanda Radio wamesema kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa migahawa hawazingazii kanuni za usafi na kuitaka serikali kuendelea kutoa elimu ili kuboresha utoaji wa huduma katika sehemu za biashara.

Aidha wakizungumza na kituo hiki wahudumu wa migahawa wamekiri baadhi ya wafanyabiashara hawazingatii kanuni za usafi huku wakiwataka wasiozingatia kuanza kuzifuata ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kulinda afya za wateja.

Katika kuhakikisha suala la usafi linakuwa endelevu Paul Swakala daktari Mganga mkuu manispaa ya Mpanda amesema hivi karibuni kwa kushirikiana na maafisa afya wataanza kufanya ukaguzi katika migahawa.