Mpanda FM

Msasani Walia na Maji Safi.

17 January 2023, 4:55 pm

MPANDA
Wananchi wa Mtaa wa Msasani Kata ya Mpanda Hotel wamelalamikia kukosekana kwa maji safi na salama kwa matumizi yao ya kila siku.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm Wamedai changamoto imekua ni ya kudumu kutokana na mabomba kuharibika mara kwa mara hali inayopelekea kukosa huduma hiyo kwa mwendelezo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Juvenali Deus amekiri kuwepo kwa kero hiyo na kuongeza kuwa ameshaandika barua MUWASA kuomba gati ya maji ila bado anasubiri utelekezaji

Aidha Diwani wa Kata ya Mpanda Hotel Khamis Msigalo amesema kuwa bomba za maji zimekua zinaharibika mara kwa mara na amewaomba watakapo kamilisha utengenezaji wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ili kukwepa kero hiyo

Msigalo amewaasa wananchi wa msasani kuwa wavumilivu wakati Maji ya Ikorongo namba tatu yanayotarajiwa kusambazwa mkoa mzima yakiwa yanasubiriwa