Mpanda FM

Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kuzinduliwa January 19 Katavi.

17 January 2023, 5:33 PM

KATAVI
Wananchi Mkoani Katavi wameombwa kujitokeza katika uzinduzi wa jengo la mahakama ya hakimu mkazi mkoani Katavi .

Wito huo umetolewa na Afisa Habari wa mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Katavi Wakili James Kapele ambapo amesema uzinduzi huo utaambatana na uzinduzi wa mahakama nyingine tatu ikiwemo mahakama ya hakimu mkazi Songwe na Lindi.

Aidha Kapele amesema uwepo wa mahakama hiyo mkoani hapa utarahisha wananchi kupata huduma ya mahakama kwa ukaribu na kurahisisha huduma kwa wananchi wa kupata suluhu ya kesi zilizokuwa zinachukua muda mrefu kukamilika na kusikilizwa.

Zoezi la uzinduzi wa mahakama hiyo linatarajiwa kufanyika January 18 2023 katika majengo ya mahakama ya wilaya kata ya ilembo mkoani hapa.