Mpanda FM

RC Katavi azindua utoaji wa chanjo ya matone ya polio awamu ya nne Wilaya ya Mlele.

2 December 2022, 3:37 pm

KATAVI
wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa chanjo ya Polio ni salama na haina madhana ya aina yoyote kwa wanao patiwa chanjo hiyo.
Mrindoko ametoa kauli hiyo  1Desemba 2022 wakati  akizindua chanjo hiyo kimkoa katika Kituo cha Afya  inyonga B Wilayani Mlele amesisitiza kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwapotosha watu juu ya chanjo mbambali zinazokuwa zinatolewa hapa nchini ikiwepo na chanjo ya POLIO.

Aidha mewahakishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa chanjo hiyo ya polio na chanjo nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa hazina madhara ya aina yoyote ile hivyo wananchi waendelee kuthamini chanjo amesema Mkoa wa Katavi utahakikisha chanjo hiyo inafanikiwa kwa zaidi ya asilimia mia moja hivyo amewataka kila mzazi anahakikisha mtoto wake anapata chanjo kabla ya kupata maradhi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Suzana Komba amesema jumla ya watoto 285, 800 watapatiwa chanjo hiyo na kwamba wamepanga kutowa huduma hiyo kwenye maeneo yanayo towa huduma na pia watapita nyumba kwa nyumba.