Mpanda FM

Wanafunzi wote mwakani mkoa wa Katavi kula chakula shuleni.

29 November 2022, 8:02 pm

KATAVI
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza wakurugenzi wa mkoa, kuhakikisha wanafunzi wote watakaojiunga na msimu mpya wa masomo mwaka 2023 wanapata chakula wakiwa shuleni .

Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa kiliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya manispaa ambapo amesema namna pekee ya kumsaidia mwanafunzi ajifunze kwa bidii nikumuwekea uhakika wa chakula pindi anapokuwa shuleni .

Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi ,Afisa elimu mkoa Dk Elipidius Baganda amesema zipo baadhi ya shule zinazo toa chakula huku akisema idara ina lengo la kuhakikisha shule zote zinatoa chakula kwa asilimia mia moja .

Mkoa wa Katavi una jumla ya shule za msingi 265 kati ya hizo shule 139 zinatoa chakula kwa wanafunzi huku shule 46 za sekondari kati ya 57 zikitoa chakula .