Mpanda FM

Katavi yajipanga kukabiliana na vitendo vya Ukatili wa kijinsia.

26 November 2022, 7:50 pm

KATAVI
Serikali mkoani Katavi imesema imejipanga katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kutoa elimu kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na afisa maendeleo ya jamii Joshua Sankala alipokuwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika mtaa wa Rungwa kata ya Kazima amesema wamepanga kutoa elimu shuleni,sokoni,makanisani na katika misikiti.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Katavi ambae ni afisa maendeleo ya jamii mkoa Anna shumbi amesema jumla ya watu 722 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na kesi 61 zililipotiwa mkoani hapa.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kujinsia hufanyika kila ifikapo November 25 na kutamatika december 10 kila mwaka ambapo kwa mwaka yamebebwa na kauli mbiu isemayo kila uhai una thamani, tokomeza mauaji na ukatili wa wanawake na watoto.