Mpanda FM

Zaidi ya Bilioni 17 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabar

25/11/2022, 4:55 AM

KATAVI
Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 17.254 kwaajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads mkoa wa Katavi Injinia Martin Mwakabende amesema mkoa umepanga kutekeleza miradi 39.

Aidha Injinia Martin amesema wakala hao bado wanakabiliana na changamoto za shughuli za kibinadamu katika maeneo ya hifadhi yanayochangia kuharibika kwa miundombinu ya barabara.

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wananchi kulinda alama zinazowekwa barabarani na kuacha kuharibu miundombinu hiyo.