Mpanda FM

Wafugaji wametakiwa kuondoa mifugo yao katikati ya mji

23/11/2022, 6:38 PM

MPANDA
Wafugaji kata ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuondoa mifugo yao na kufugia nje ya mji.

Katazo hilo limetolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Kashaulili Merry Ngomarufu ambapo amesema wafugaji wote wenye mifugo iliyopo katika kata hiyo tayari wameshapewa utaratibu ili kuondoa mifugo yao katikati ya mji na kwenda kufuga pembezoni mwa mji.

Merry ameongeza kuwa sababu ya kutaka wafugaji kuondoa mifugo ni uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mifugo hiyo.

Aidha amebainisha kuwa kwa wafugaji wote watakao kiuka agizo hilo na kukamatwa mifugo yao watachukuliwa hatua za kisheria,na kutoa faini ya shilingi laki tatu.