Mpanda FM

Wafanyabiashara wametakiwa kulipa Ushuru

23/11/2022, 5:47 PM

MPANDA
Wafanyabiashara Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kutoa ushuru kikamilifu,ili fedha hizo ziweze kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwamo ya elimu na afya.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sofia Kumbuli ambapo amesema kuwa swala la malipo ya ushuru wa maegesho ni takwa la kisheria hivyo wahusika wanapaswa kuwajibika kulipa ushuru huo bila kulazimishwa .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameitaka ofisi ya mkurugenzi kujikita zaidi katika utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa kulipa ushuru

Hivi karibuni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imeanzisha ushuru wa kodi ya maegesho kwa vyombo vya moto ikiwemo magari ,Bajaji na pikipiki lengo ikiwa ni kuongeza chanzo cha mapato ya ndani .