Mpanda FM

Wanawake Mkoani Katavi Wameeleza Walivyonufaika na Wiki ya Mwanakatavi

03/11/2022, 5:58 AM

KATAVI

Baadhi ya wanawake wajasiliamali mkoani Katavi wameeleza namna ambavyo wamenufaika na maonesho ya wiki ya Mwanakatavi yanayolenga kuhamasisha kilimo na Utalii.

Wakizungumza wakati wa maonesho hayo wajasiliamali hao wamesema maonesho hayo licha ya kuwanufaisha kibiashara pia wanapata nafasi ya kujua fursa zinazopatikana mkoani hapa.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph Kimaro  amewapongeza wanawake hao kwa kuwa wajasiliamali huku akitoa ufafanuzi namna ambavyo wanaweza kunufaika kupitia vikundi ili kupata mikopo ya 10%.

Maonesho ya wiki ya mwanakatavi yanatarajiwa kutamatika Novemba 02 mwaka huu.