Mpanda FM

Diwani Mpanda Hotel Aomba Kurejeshwa kwa Utaratibu wa Maegesho Mpanda Hotel.

03/11/2022, 5:35 AM

MPANDA

Diwani wa kata ya Mpanda Hotel Hamis Misigalo ameiomba halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kurejesha utaratibu wa Magari ya abiria kusimama dakika tatu katika kituo cha maegesho ya magari Mpanda Hotel.

Akizungumza katika Mkutano wa Tatu wa baraza la madiwani Misigalo amesema kuwa kitendo cha magari ya abiria kutokupaki katika eneo hilo imekuwa adha kwa wafanyabiashara wa eneo hilo..

Akijibu hoja hiyo kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu amemtaka diwani huyo kukubaliana na maamuzi ya Halmashauri ya kuzuia maegesho katika eneo hilo huku akibainisha kuwa moja ya sababu ni kuwepo kwa ajali za mara kwa mara ambazo zinapelekea wananchi kupoteza Maisha.

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imezuia magari ya abiria kupaki katika maegesho ya magari ya Mpanda hoteli huku ikibainisha kuwa ni kwaajili ya maslahi mapana ya wananchi.