Mpanda FM

Wananchi Waaswa Juu ya Tahadhari ya Magonjwa ya Mlipuko

21 October 2022, 11:10 am

MPANDA

Wananchi  Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya milipuko ikiwamo kuhara kwa kunawa mikono na maji tiririka na sabuni sambamba na kutibu maji ya kunywa.

Afisa afya Manispaa ya Mpanda Erick Kisaka ameitaka jamii kuchukua tahadhari kwa kuzingatia usafi na usalama wa mikono kwa kutumia kitakasa mikono pamoja na kunawa Mikono kwa maji tiririka  na sabuni kutokana na magonjwa mengi ikiwamo Kipindupindu ,Ebola, Uviko 19.

Kwa upande wake Beuty Mwambebure kutoka wizara ya Afya amesema jamii inapaswa kuchukua tahadhari kwa kutumia maji safi ya kunywa ambayo yametibiwa kwa kuwekwa dawa au kuchemshwa ili kuepukana na magonjwa ya matumbo na kuhara.

Wizara ya afya nchini imeendelea kutoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya magonjwa ya mlipuko ambayo pia yanaripotiwa kuzikumba nchi jirani.