Mpanda FM

Wafanyabiashara Kilimahewa Waomba Kuboreshewa Miundombinu

20/10/2022, 5:11 AM

MPANDA

Wafanyabiashara wa soko la kilimahewa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameuomba uongozi wa halamshauri hiyo kuboresha miundombinu katika soko jipya la kawalioa.

Wakizungumza na Mpanda fm wafanyabiashara hao wamesema  kuwa licha ya kuwepo kwa taarifa ya kuhamia katika soko jipya la kilimahewa lakini miundombinu ya kufanyia biashara bado sio rafiki kwao.

Kwa upande wake Afisa habari wa manispaa ya mpanda Dornald Pius  akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo amesema kuwa wafanyabiashara hao wanapaswa kuhamia katika soko jipya lililotengwa na serikali huku miundombinu ikiendelea kuboreshwa.

Tarehe 15 mwezi October mwaka huu wafanyabiashara hao wa soko la Kilimahewa walipewa taarifa ya kuhamia katika Soko jipya la kawalioa kwa muda wa siku mbili mbaka kufika jumatatu ya Oct 17,2022.