Mpanda FM

Tanesco Wapewa Wiki Tatu Kufikisha Umeme Hospital Mpya ya Mkoa

20 October 2022, 5:24 am

MPANDA

Mkuu wa mkoa wa Katavi  Mwanamvua Mrindoko amewataka Shirika la umeme mkoa wa Katavi ndani ya wiki tatu kuhakikisha umeme unafika katika hospitali mpya ya mkoa wa Katavi

Akitoa maagizo wakati akijibu taarifa ya mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa, mkuu wa mkoa wa Katavi amesema wanapaswa kutekeleza agizo hilo ili kuwapunguzia wananchi adha ya kupata rufaa ya Kwenda hospital kubwa kutokana na vifaa vilivyowekwa  nan kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya kukosa umeme unaohitajika.

Awali akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa hospital mpya ya mkoa  Dk Seraphine Patrice amesema baaadhi ya mnajengo yameshakamilika na mitambo ishawekwa huku changamoto ni upatikanaji wa umeme.

Kwa mujibu wa maelekezo ya serikali yaliyotolewa na serikali chini ya wizara ya afya  mwezi wa 9 mwaka huu hospital hiyo inapaswa kuanza kufanya kazi tarehe 14/11/2022.