Mpanda FM

Wajasiriamali Walalamikia Wateja Wasiowaaminifu

14/10/2022, 5:51 AM

 

MPANDA

Wajasiriamali Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelalamikia Tabia isiyofaa inayofanywa na baadhi ya wateja ya kuchukua bidhaa kwa mkopo na kuchelewa kuwalipa jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo yao kiuchumi.

Wakitoa malalamiko hayo wakati wakizungumza na kituo hiki wajasiliamali hao wamesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wateja kuhitaji bidhaa pasipo kuwa na pesa tasilim na kuahidi kuwalipa na kujikuta wakienda kinyume na makubaliano .

Kwa upande wa wananchi wametoa maoni yao na kusema kuwa tabia hiyo si nzuri na inasababisa kuleta athari kwa wajasiliamali hao kwani wanarudishwa nyuma kimaendeleo.

Aidha wamewataka vijana  kujikita katika shughuli za ujasiliamali ili waweze kuwa na kipato na kuondokana na vitendo vya udokozi na wizi.